18 Aug

Na Mtu Ni Afya,Njombe

Wakazi wa Kata ya Kidengembe waazimia kufanya kweli kwa kuzungumza masuala yahedhi salama na kuvunja ukimya katika ngazi ya kaya kwa kuwashirikisha wanaume namabinti zao.

Azimio hilo limewekwa na wakazi wa Kata ya Kidengembe pamoja na Mganga Mkuu waHalmashauri ya Njombe Frank Mganga wakati wa mahojiano maalumu na timu ya MtuNi Afya.

Mganga Mkuu, amesema wakina mama wanatakiwa kukaa na mabinti zao,kuwashirikisha na kuwapa nafasi ya kujielezea juu ya mabadiliko ya ukuaji.

Mkazi wa Kata ya Kidengembe, Eliud Mtato ameomba wakina mama kufanya kweli kwakushirikisha wanaume zao juu ya masuala ya hedhi salama kwakuwa hedhi salama nijukumu la kila mtu.

Katika hatua nyingine, Mganga Mkuu, amesema katika afua ya vyoo bora, Serikali yaNjombe imekuwa ikienda kuanzia ngazi ya kaya mpaka taasisi na kuonyesha ujenzi wavyoo bora vya mfano.