04 Oct

MKUU wa Wilaya(DC) ya Kibiti mkoani Pwani, Joseph Kolombo amewataka wakazi wa Wilaya ya Kibiti kufanya kweli kwa kujengavyoo bora pamoja na sehemu ya kunawia mikono na maji tiririka.

Kolombo amesema hayo jana ofisi kwake wakati wa mahojianomalumu.

‘’Ujenzi wa vyoo bora ni ajenda yangu namba moja nimeshawaelekezawakazi wa Kibiti kufanya kweli kwa kujenga vyoo bora. Ujenzi wa vyoobora ni lazima iendane na sehemu nzuri ya kunawia mikono’’ amesema.

Katika hatua nyingine, Kolombo ameahidi kuendeleza kuhimiza wakaziwa Kibiti kutobaki nyuma katika suala zima la kufanya mazoezi.

‘’ Licha ya wananchi wengi kutopenda mazoezi, tutaendeleakuwahimiza kufanya kweli katika ufanyaji wa mazoezi mara kwa marahii itasaidia sana kuepuka magonjwa yasioambukizwa pamoja na mwilibwete’’ amesema.

Naye Afisa Mtendaji wa kata ya Kibiti, Ammy Ally amesema kata yaoinafanya kweli kwa kuondokana na matumizi ya kuni pamoja na vifuu. Amesema wakazi wengi kwa sasa  hawajabaki nyuma katika kutumianishati safi ya kupikia.

‘’Katika kipindi cha nyuma, wakazi wengi wa Kibiti walikuwawanatumia kuni, vifuu ili kwa sasa wengi wameamua kufanya kwelikwa kutumia nishati safi ya kupikia’’ amesema.