14 Oct

WAFANYABIASHARA wa soko la samaki la Dunda katikaHalmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wamefanya kweli katika kutumianishati safi ya kupikia.

Akizungumza na Mtu Ni Afya jana katika soko hilo,Katibu mkuu wasoko la samaki la Dunda, Haji Sudi amesema wafanyabiashara wa sokolao wameamua kutobaki nyuma katika matumizi ya nishati safi yakupikia.

‘’Kwa pamoja, tumeamua kufanya kweli kwa kuacha kutumia kuni namkaa, tumeona ni vyema kutumia gesi katika kupikia.Awaliwafanyabiashara walikataa kutumia gesi lakini kwa sasa ni wotewameamua kutumia majiko ya gesi’’ amesema.

Naye balozi wa kampeni ya Mtu Ni Afya, Mrisho Mpoto amewapongezawafanyabiashara wa soko hilo kwa kufanya kweli na kutumia nishatisafi.

‘’Soko la samaki la Dunda, wameamua kufanya kweli kwa kuacha nanishati isiyokuwa safi(Mkaa na kuni) na hawajabaki nyuma katikakutumia nishati safi ya kupikia ya gesi’’ amesema.

Katika hatua nyingine, Afisa Mtendaji wa kata ya Dunda,JudithMayunga amesema katika kufanya kweli, maeneo soko la Dundayamewekewa sehemu ya kumwagia takataka kwa lengo la kutobakianyuma katika kutunza Mazingira.

‘’Tumefanya Kweli kwa kuongeza sehemu za kutupia takataka. PiaUsafi wa Mazingira huwa tunafanya kwa pamoja kila jumamosi’’ amesema.