16 Dec

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetoa pongezi kwa Chuo Kikuu Cha Afya na SayansiShirikishi Muhimbili(MUHAS) kwa mpango wa kujenga kituo Jumuishi cha michezo katikakampasi ya Muhimbili, jijini Dar-es-salaam.

Pongezi hizo zilitolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dkt NtuliKapologwe wakati wa kufunga mbio za Reunion Fun Run msimu wa Tatu. Dkt Kapologweamesema kituo hicho jumuishi cha michezo kitasaidia kuhamasisha ufanyaji mazoezi katikajamii.

‘’Sisi kama Serikali, Tumeungana na Muhas kwajili ya kuhamasisha kampeni ya Mtu ni Afya, huu ni utaratibu mzuri wa kufanya mazoezi sisi kama Wizara ya Afya tumekuwa tukihamasishavyuo, Idara mbalimbali kuwa na utaratibu mzuri wa kufanya mazoezi’’ amesema.

Dk Ntuli amesema Mbio hizi siyo tu zitahamasisha mazoezi, bali pia zinasaidia kukabiliana namagonjwa yasiyoambukiza.

Mbio hizi siyo tu zinahamasisha mazoezi, bali pia zinasaidia kukabiliana na magonjwayasiyoambukiza kama shinikizo la damu, kisukari, na magonjwa ya moyo. Hii ni sehemu yakampeni ya Fanya Kweli Usibaki Nyuma inayolenga kuhakikisha kila mtu anajali afya yake,” amesema Dkt. Kapologwe.