
CHUO Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Muhimbili ipokatika mpango wa kujenga kituo Jumuishi cha Michezo kwa lengo la kuhimiza ufanyaji mazoezikatika jamii. Rai hiyo imetolewa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa ApolinaryKamuhabwa wakati wa kuhitimisha mbio za Reunion Fun Run msimu wa tatu zilizofanyikakatika viwanja vya Muhimbili.
‘’Lengo kubwa ni kutafuta rasilimali fedha ili tuweze kujenga kituo cha michezo katika kampasiya Muhimbili.Wote tunahitaji kituo cha michezo kwajili ya wafanyakazi wa Hospitali yaMuhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Taasisi yaSaratani ya Ocean Road ,wanafunzi wa Muhas na wafanyakazi wa chuo hicho , wananchi waDar es Salaam na wagonjwa watakaokuwa na nafuu na wenye kuhitaji mazoezi.’’ Amesema.
Akielezea zaidi kuhusu ujenzi wa kituo cha Michezo, Profesa Kamuhabwa amesema ujenzi wakituo hicho cha michezo unatarajia kuanza mwakani 2025. Amesema kituo hicho kitakuwa nauwanja wa mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa kikapu pamoja na sehemu ya Mazoezi yaviungo(GYM). Amesema pia kutakuwa na vyumba vya kubadilishia nguo pamoja na vyoo.
Amesema jamii imekuwa inakabiliwa na changamoto ya kutokufanya mazoezi jambolinalopelekea kuongezeka kwa magonjwa yasioambukizwa kama shinikizo la damu na kisukari.
Profesa Kamuhabwa amesema chuo chao kina shule ya Afya ya jamii kwa lengo la kuhamasishaAfya bora katika jamii na umuhimu wa kufanya mazoezi.