
Hedhi salama ni suala muhimu sana kwa ustawi wa afya ya wasichana na wanawake. Hata hivyo, katikajamii nyingi za Tanzania, changamoto zinazohusiana na hedhi salama bado zipo. Ni jukumu la kila mzazikumuelimisha mtoto wake kuhusu masuala ya hedhi salama.
Kwa upande mwingine, jamii kubwa ya wakina baba imekuwa ikishindwa kushiriki katika majadilianokuhusu hedhi, hali inayofanya jukumu hili kuwa la kina mama pekee. Mila na desturi nyingi zimewafanyababa wa familia kuwa mbali na majadiliano haya muhimu, na hivyo kuendeleza hali ya ukimya na aibuinayozunguka mada hii.
Ili kuboresha hali hii, ni muhimu kwa wanawake kuwapa nafasi wanaume kuungana na kushiriki kikamilifukatika kuhakikisha kwamba kila msichana na mwanamke anapata taarifa sahihi na uelewa kuhusu hedhisalama. Hedhi salama inajumuisha uwepo wa miundombinu inayowezesha tabia ya hedhi salama, kamavile vyumba vya kubadilishia taulo, upatikanaji wa maji safi, na sehemu maalum za kuchoma taulozilizotumika.
Jamii, ikiwa ni pamoja na baba, inapaswa kuacha ukimya kuhusu hedhi na badala yake iwe namajadiliano ya wazi kati ya wazazi na watoto wao, bila kuwasahau watoto wa kiume. Watoto wa kiumepia ni sehemu muhimu katika kufanikisha hedhi salama; ikiwa wataweza kuwa na taarifa sahihi kuhusuhedhi, watasaidia kuondoa unyanyasaji wa kijinsia kati yao na watoto wenzao wa kike.
Ili kufikia maendeleo endelevu, jamii inapaswa kujitambua na kila mmoja kufanya kweli kwa manufaa yajamii kwa ujumla. Hili litawezesha mazingira bora ya hedhi salama na kusaidia kuboresha ustawi wa afyaya wasichana na wanawake, hivyo kuchangia katika maendeleo ya jamii nzima.