10
Jul
JAMII imeshauriwa kuweka utaratibu malumu wa kutunza mazingira katika maeneo yao ya nyumbani na kazini.
Witu huo umetolewa na Mkuu wa kitengo cha Afya kutoka Jukwaa la Vijana kusini wa Afrika(SADC) Vivian Joseph wakati Kongamano la wadau wa sekta ya Afya kuhusu maandalizi ya Dira ya Taifa ya maendeleo 2050liliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere(JNICC).
Amesema umuhimu wa kusafisha Mazingira unasaidia katika kutunza taka katika sehemu inayotakiwa. Amesema jukumu la kutunza Mazingira ni la kila mmoja.
Akielezea kuhusu hedhi salama, Vivian amepongeza juhudi za Serikali kwa kuondoa kodi katika taulo za kike jambo ambalo linasaidia katika upatikanaji wake.
Katika hatua nyingine,amewashauri vijana kuweka ratiba maalumu ya kufanya mazoezi angalau kwa nusu saa kwa siku.
Kwa upande wake Mwanafunzi wa masomo ya udaktari kutoka Chuo cha Sayansi shirikishi Muhimbili(MNH) Jerome Jumanne amesema Shirika la Afya Duniani(WHO) kwa takwimu zake zinaonyesha baada ya miaka 50 ijayo,magonjwa yasiokuambikiza ni magonjwa tutakayokabiliana nayo.
Akielezea kuhusu sababu ya magonjwa hayo, Jumanne alisema magonjwa hayo yanasababishwa sana na maisha yetu ya kila siku.
Ameshauri Jamii iwe na utaratibu malumu wa ufanyaji mazoezi ili kujiepusha na magonjwa kama Kisukari, uzito mkubwa na presha.
Mwisho