
MKUU wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, Nickson Simon amesema Wilaya yao itaendeleakutenga bajeti ya utunzaji na usafi wa Mazingira. Simon amesema hayo jana wakati wamahojiano malumu.
‘’Sisi kama Wilaya ya Kibaha,tunafanya kweli katika usafi wa Mazingira ambapo kamaHalamshauri huwa tunatenga bajeti ya usafi. Pia tumefanikiwa kutenga bajeti ya nishati safi ‘’ amesema.
Amezishauri pia familia ziweze kutenga bajeti ili kufanya kweli katika kununua pedi za watotowa kike na wasibaki nyuma katika hedhi salama.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha,Salum Ally amesema upande wanishati safi hawajabaki nyuma kwakuwa Halmashauri yao huwa inawapa wakazi wake majiko yagesi kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati.
Amewaomba pia wazazi wasibaki nyuma katika kuwafundisha watoto wao kuhusu hedhi salama. Ally amesema pia huwa wanafanya kampeni
‘’Hedhi salama sio siri, ni wakati sasa wazazi kuacha kuona aibu bali wanatakiwa kuwafundishawatoto wao jinsi ya kutumia pedi pamoja na kuzihifadhi pedi hizo katika chombo malumu iliwasichafue mazingira’’