
MKUU wa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, Khadija Nassir amewataka wazazi wotewilayani Mkuranga kufanya kweli kwa kuwa na utaratibu wa kuzungumza watoto wao kuhusuelimu ya Hedhi salama. Nassir ametoa rai hiyo jana wakati wa mkutano katika stendi ya Kimanzichana.
‘’Ni jukumu letu, Wazazi tuongelee Hedhi salama bila uwoga. Takwimu zinasema mabinti wengi wanakosa masomo yao wakiwa katika kipindi cha hedhi. Ni wakati sasa tusibaki nyuma katika suala hili’’ amesema.
Amesistiza Wazazi kutoficha kuhusu hedhi salama kwakuwa jambo hilo bado ni changamoto kwa wilaya yake.
Katika hatua nyingine, Afisa Mtendaji wa kata ya Mkuranga, Elizabeth Shirima amewaagiza wafanyabiashara wa soko la Mkuranga kuzingatia na kutunza usafi wa Mazingira.
‘’Ni wakati sasa wafanyabiasahara wa soko la Mkuranga pamoja na wakazi wa Mkuranga kutobaki nyuma katika kufanya usafi. Watu waache uzembe na kufanya kweli katika usafi’’ amesema.
Naye Mwenyekiti wa soko la Mkuranga,Shaishi Mohamed amesema kwa soko lao wanafanya kweli kwa kufanya usafi kila siku pia hawajabaki nyuma katika kufanya usafi wa pamoja katika ya wafanyabiashara wa soko la Mkuranga na stendi.
‘’Usafi ni wajibu wetu, kufanya kila siku sio mpaka kampeni za usafi zije katika soko letu ndio tufanye usafi’’ amesema Mohamed.
Mwisho