
MKUU wa mkoa wa Iringa Peter Serukamba amewakumbusha wakazi wa mkoa wake kufanyakweli katika ufanyaji wa usafi wa Mazingira. Serukamba ametoa wito huo jana wakati wamahojiano malumu.
‘’Hakika sisi watu wa Iringa, hatubaki nyuma, tunaendelea mbele na tutafanya kweli. Piakufanya usafi ni sehemu ya maisha yetu’’ amesema.
Serukamba amesema katika kuhakikisha hawabaki katika usafi wameunda kamati malumu zakusimamia usafi kuanzia ngazi ya Halmashauri mpaka mkoa.
‘’Tumeunda kamati kuanzia ngazi ya Halmashauri mpaka mkoa na kila baada ya wiki mbilitunakutana mkoani kwajili ya kuja kuripoti kinachoendelea kwenye eneo la usafi kwa kilaHalmashauri. Kampeni hii tumeiwekea miundo mbinu ya kusimamia kuhakikishainatekelezwa’’amesema.
Kwa upande wake Afisa utamaduni wa mkoa wa Iringa,Steven Sanga amesema kwa upande waufanyaji wa mazoezi, mkoa wa umeweka utaratibu malumu wa kufanya kweli kwa kufanyamazoezi kila Jumamosi.
‘’Mkoa wa Iringa, tumekuwa na mazoezi yanayofanyika kila Jumamosi kwa watumishi, wananchi na wafanyakazi wa taasisi mbalimbali’’ amesema.
Akielezea zaidi, Sanga amesema mazoezi wanayofanya ni kukimbia pamoja na kutembeaambapo mazoezi huanzia kwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa mpaka Kihesa-Kilolo.